Idadi ya waliofariki kwa ajili ya Covid 19 yafika 664 baada ya watu 5 zaidi kufariki

Visa vipya 130 vya covid 19 vimeripotiw anchini na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa  37,348 ,  amethibitisha waziri wa Afya Mutahi Kagwe .

Visa hivyo ni kutoka sampuli 3,874 zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita  na kufikisha jumla ya sampuli zilizopimwa hadi sasa kuwa 523 .998 .

Kiwango cha maambukizi sasa kipo asilimia 3.34.

Visa vyote ni vya  wakenya isipokuwa  saba ambao ni raia wa kigeni .

Watu watano Zaidi wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioangamizwa na ugonjwa huo nchini kuwa 664 .

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema mgonjwa wa umri wa chini ana miaka mitatu ilhali wa umri wa juu ana miaka 90 .

Nairobi inazidi kuongoza kwa visa vingi baada ya visa 35 kusajiliwa katika saa 24 zilizopita Kiambu (23), Kisumu (19), Mombasa (14), Uasin Gishu (8), Kerich (6), Kisii (5), Busia (5), Kilifi (5), Bomet (2), Narok (2), Siaya, Trans Nzoia, Turkana, Kajiado  na  Machakos  zikiwa na kisa 1 kila moja

Watu wengine 106 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo nchini kuwa  24 ,253 .