Kiti hicho kiliachwa wazi baada ya kifo cha Suleiman Dori wa ODM.
Jubilee imesema kwa sababu ya ushirikiano wake na ODM hakitaweza kuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo .
Chama hicho kimesema taifa kwa sasa linapitia mambo mengi ikiwemo ushauri wa jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge .
" Kwa sasa nchi inapitia mengi na tunahitaji ukomavu ili kuyashughulikia ikiwemo kuziba mianya katika mirengo ya kisiasa’. Amesema katibu mkuu wa chjama hicho Raphael Tuju
Ameongeza ‘ Uamuzi huu umetolewa kwa wakati ufaao ili iwapo kuna mgombeaji wa Jubilee aliyetaka kiti hiki basi awe na njia mbadala za kugombea’
Wakaazi wa eneo bunge hilo watamchagua mbunge mpya disemba tarehe 15 baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa sababu ya janga la corona .