MCA avunjwa mkono katika makabiliano bungeni kuhusu hoja ya kumfurusha gavana Obado

MIGORI
MIGORI
Mwakilishi  mmoja wa  kaunti  amevunjwa mkono katika patashika  ndani ya bunge la kaunti ya Migori  kabla ya kuwasilishwa kwa hoja ya kumuondoa afisini gavana Okoth Obado .

Mwakilishi mteule Mary Ogodo  alivunjika mkono wake wa kushoto  baada ya kizaazaa kuzuka katika bunge hilo  kwa sababu ya mgawanyiko kuibuka kuhusu hoja ya kutaka kumuondoa madarakani gavana Obado .

Patashika hiyo ilimfanya  Sajini mkuu kukimbia  na kifaa cha maamlaka ya bunge  m na kuwacaha waakilishi wengine wakipambana na wenzao katika bunge la kaunti huku chupa za maji zikirushwa na viti vikitumiwa kama silaha .

Ogodo  alikimbizwa katika hospitali ya  kimishenari ya St Joseph  ambako anapokea matibabu .

Malumbano yalianza  wakati wa kikao cha asubuhi wakati mwakilishi wa wadi ya  North Kanyamkago George Omamba alipopata agizo kutoka kwa mahakama kuu ya Mgori kumrejesha kama naibu wa spika .

Omamba alikuwa amefurushwa na wenzake kupitia kura mwaka jana  pamoja na karani wa bunge  Tom Opere  huku  mwakilishi wa wadi ya  Bukira mashariki  Mathews Chacha  na Emmanuel  Abala wachukua hatamu kwa muda

Malumbano yalizuka wakati waakilishi watano wanaomuunga mkono Obado wakiongozwa na   mwakilishi wa Kaler  Thomas Akungo  walipoingia bungeni na kujaribu kukatiza kikao kilichokuwa kikiendelea .