NMG yaagizwa kuitoa mtandaoni taarifa ya upekuzi ya 'Covid Millionaires'

covid milionaires
covid milionaires
Mahakama kuu imeagiza kauni ya NMG  Kkuondoa mtandaoni taarifa ya upekzi ya  ‘Covid-19 Millionaires’  hadi kesi iliyowasilishwa dhidi yake isikizwe na kuamuliwa .

 Katika kesi hiyo  , Megascope Ltd  iliwasilisha kesi kortini kuishtaki NMG na mwanahabari  Dennis Okari  kwa kuihusisha na  sakata katika shirika la Kemsa na hivyo basi kuiharibia jina kampuni hiyo .

Jaji  Joseph Sergon  jumatano ametoa agizo la kuitaka NMG kuindoa taarifa hiyo mitandaoni baada ya Megascope kuwasilisha ombi hilo  hadi kesi hiyo sikizwe na kuamuliwa .

 Taarifa hiyo ya upekuzi  iliwekwa Youtube na kufikia sasa ilikuwa imetazamwa mara 700,000

Wakili wa   megascope  Njoroge Regeru alikuwa ametoa ombi kwa jaji  akisema taarifa hiyo   kuslaia katika mitandao ya kijamii iliendelea kuharibu sifa za kampuni ya mteja wake . Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na wakili wa NMG Kiragu Kimani  akisema maagizo yaliyotolewa  hapo awali kwamba wasiandike taarifa zaidi kuihusu megascope na sakata hiyo yalitosha .

Kesi hiyo itatajwa Oktoba tarehe 22 .