Sikujua kama kipindi cha Selina kitakuwa kikubwa hivi-Pascal Tokodi

Muigizaji na mwanamuziki Nelson almaarufu Pascal Tokodi anafahamika sana kwa sauti yake na hata uigizaji wake,akiwa kwenye mahojiano muigizaji Pascal alizungumzia jinsi alipata uigizaji katika kipindi cha Selina ambacho hupeperushwa katika runinga ya maisha magic east kila juma ya wiki.
"Walikuwa wanatafuta muigizaji Nick Mutuma ambaye ni rafiki yangu aliniambia nikiwa Mombasa nikiwa kazini nilikuwa naigiza kitu fulani

Aliponipigia nilisema kama huo uigizaji ni wangu basi ni wangu na kama si wangu utapata mwingine basi, baada ya siku chache alinipigia simu akaniambia kuwa hawajapata muigizaji ambaye wanamtaka napaswa kuenda katika ukaguzi nilipoenda nilichaguliwa

Kipindi cha Selina nitahishi kukishukuru maishani mwangu, kwa maana kimenikuza na hata nimesoma mambo tofauti, sikujua wala kufahamu kama kipindi hicho kitakuwa kikubwa hivyo

katika kipindi hicho kitu ambacho nimeigiza nikajivunia ni wakati ambao nilikuwa naigiza nikilia." Alieleza Pascal.

Pascal ameshinda tuzo nyingi katika uigizaji na hata katika sanaa ya muziki, huku akizungumza hayonalidai ya kwamba wanawake wengi wanapenda sauti yake kulivyo anavyoipenda.

Muigizaji huyo pia alisema kuwa wazazi wake walimuunga mkono katika kazi yake ya uigizaji na hata kumpa msukumo mkubwa.