Wabunge waidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kama msajili wa vyama vya kisiasa

ANN NDERITU
ANN NDERITU
Kamati moja ya bunge siku ya alhamisi  imeidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kama msajili wa vyama vya kisiasa .

Nderitu  amekuwa  akishikilia nafasi hiyo kwa muda tangu mwaka wa 2018  alipochukua usukani kutoka kwa Luvy Ndung’u  aliyehamia tume ya Haki

Jamati ya haki na masuala ya sheriapia imewaidhinisha  Ali Abdullahi na  Florence Tabu  kama manaibu wa msajili wa vyama

Kamati hiyo inayoongozwa na  Kigano Muturi  hata hivyo imekataa kumwidhinisha Wilson Mohochi kama naibu wa msajili

Rais Uhuru Kenyatta  alimteua Nderitu kuchukua kazi hiyo Septemba tarehe 8  .Kabla ya kuichukua akzi hiyo Nderitu alikuwa mkuu wa usajili wa wapiga kura katika tume ya uchaguzi.