'Corona ilisimamisha Reggae ya BBI,'Murkomen amjibu mbunge Opiyo

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amejibu ujumbe wake mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi uliosoma kuwa ni masikitiko makubwa kuwa viongozi wa serikalini wameanza kampeni za siasa mapema.

Kwa mujibu wake Murkomen alisema kuwa janga la corona lilisimamisha wimbo wa reggae wa BBI, na kuwa BBI ilibadilisha hali ya wananchi wa Kenya.

"Mikutano ya BBI iliunda hali ya humu nchini kwa muda mrefu uliopita, na kwa sababu ya corona reggae ilisimama." Murkomen Alijibu.

Usemi au majibu yake yalijiri baada ya mbunge Opiyo kusema kuwa nchi iko katika hali ya kampeni za kisiasa ambapo imesalia mwaka mmoja na nusu.

"Ni kwa bahati mbaya kuwa nchi hiko katika hali ya kampeni za kisasa karibu mwaka mmoja na nusu ili uchaguzi mkuu kutimia jambo mbaya zaidi ni kuwa wanaofanya hali hii kutendeka ni viongozi wa serikalini na kutumia pesa za walipa kodi." Aliandika Opiyo.