- Kocha wa Inter Milan Antono Conte amtaka Sergio Aguero
- Memphis Depay hajafutilia mbali uwezekano wa kuhamia Barcelona mwezi januari
- Mfaransa Houssem Aouar, 22, anaamini kusalia Lyon ni uamuzi ufaao
Kocha wa Inter Milan Antono Conte anapanga kuwasilisha ombi la kumsaini mchezaji wa Manchester City na raia wa Argentina Sergio Aguero, 32, ambaye mkataba wake utatamatika mwishi mwa msimu huu
Kilabu ya Bournemouth imekataa ofa kutoka kwa West Ham kumsajili mshambuliaji wa Norway Joshua King mwenye umri wa miaka 28 kwa pauni milioni 13. Hata hivyo the hammers bado ipo katika mazungumzo na Brentford kumsaini Said Benrahma mwenye umri wa miaka 25 raia wa Algeria
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester Memphis Depay hajafutilia mbali uwezekano wa kuhamia Barcelona mwezi januari . mshambuliaji huyo wa Uholanzi alisalia Lyon ili kukamilisha mwaka mmoja katika mkataba wake lakini kilabu hiyo ya Ufaransa ina chaguo la kumuuza katika kipindi kijacho cha uhamisho
Mchezaji mpya wa man United Facundo Pellistri, raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 18 anapanga kurejea nyumbani kwao kwa kujiunga na kilabu ya Penarol, ambaypo aliondoka ili kujiunga na Old Trafford.
Manchester City imeamua kusalia na huduma za mlinzi wa Uhispania Eric Garcia kwa kipindi cha msimu huu kwa sababu ana thaani ya juu kuliko pauni milioni 18 ambazo Barcelona imetoa kama ofa ya kumnunua . Garcia mwenye umri wa miaka 19 anaweza kuelekea Nou Camp kipindi kijacho bila malipo yoyote baada ya kudinda mkataba mpya .
Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amesema mshambuliaji wa Luis Suarez, 33, angesalia Nou Camp ili kumdhihirishia ubabe wake uwanjani badala ya kutorokea Atletico Madrid.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool na England Daniel Sturridge, 31, anaamini kwamba kurejea kwake katoka soka sasa hakuwezi kuepukika baada ya mkataba wake na kilabu ya Uturuki Trabzonspor kukatizwa kwa makubaliano ya pande zote mbili mwezi machi na katika siku hiyo alipokea marufuku ya miezi minne kwa kukiuka sheria za michezo ya kubashiri .
Difenda wa Denmark Joachim Andersen amesema maneja Scott Parker alimshawishi ajiunge na Fulham .Torino pia imekuwa ikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 .
Kiungo wa kati Mfaransa Houssem Aouar, 22, anaamini kusalia Lyon ni uamuzi ufaao baada ya kuhusishwa pakubwa na uwezekano wa kuhamia Arsenal