Covid-19: Visa 604 vipya vya maambukizi ya corona vyarekodiwa huku 10 wakifariki

Muhtasari

•Watu 10 waaga dunia kutokana na corona

•Visa 604 vya rekodiwa nchini hii leo huku 88 wakipona

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Visa 604 vipya vya maambukizi ya virusi vya corona vya rekodiwa humu nchini huku idadi hiyo ikifa jumla idadi ya 42,541, hii ni kutokana na sampuli 5,832 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Kati ya visa hivyo vipya 583 ni wakenya huku 21 wakiwa ni raia wa kigeni, 400 ni wanume ilhali 204 ni wanawake.

Mgonjwa umri wa chini ana miezi mitano huku mwenye umr wa juu akiwa na miaka 94 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

 

Huku hayo yakijiri watu 88 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 31,428 ya watu waliopona kutokana na corona.

Vile vile watu 10 hii leo wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 797 ya watu walioaga dunia.