kisa ni nini? Moto wateketeza bweni la shule ya upili ya Musingu

oparanya
oparanya

Moto mkubwa ulizuka katika shule ya upili ya wavulana ya Musingu ilio katika kaunti ya Kakamega.

Nduru za habari zili harifu ya kwamba moto huo uliteketeza bweni moja wa shule hiyo, huku wanafunzi wakisema ya kwamba waliona moshi katika eneo hilo.

Chanzo cha moto huo hakikubainika, huku kisa hicho kikitokea siku mbili baada ya shule kufunguliwa baada ya kufungwa kwa muda wa miezi sita baada ya janga la corona kukita kambi humu nchini.

Masoma yalikatizwa kwa saa kadhaa wakati moto huo ulizuka Kufikia sasa, hakuna majeruhi ambayo yameripotiwa.

Mwaka wa 2019, mikasa miliwi ya moto ilishuhudiwa shuleni humo, mkasa wa pili ukiwa mwezi Novemba 2019.

Gavana Oparanya anatarajiwa kutembelea shule hiyo.