DP Ruto aahirisha mkutano wake wa Murang'a ili kuhudhuria kikao cha rais

Muhtasari
  • Naibu rais William Ruto aihirisha mkutano wake wa Murang'a
  • Mkutano huo uliahisrishwa ili kuhudhuria mkutano wa rais Uhuru Kenyatta.
Ruto
Wiliam Ruto Ruto
Image: Maktaba

Naibu Rais William Ruto ameahirisha hafla ya mchango iliyokuwa imeratibiwa kufanyika hapo kesho kaunti ya Murang'a ili kumuwezesha kuhudhuria mkutano wa Rais Uhuru Kenyatta.

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, ambaye alikuwa mmoja wa waandalizi wa harambee hiyo, alitangaza hatua hiyo Alhamisi Oktoba 15.

Nyoro alisema harambee hiyo ilikuwa ifanyike Ijumaa, Oktoba 16 lakini ikaahirishwa baada ya Rais kuita mkutano wa baraza la mawaziri.

"Tumeahirisha harambee iliyokuwa imepangwa kufanyika kesho Mathioya na Kangema hadi Oktoba 30. Hii ni kutokana na mkutano wa baraza la mawaziri unaoanza leo jioni na kuendelea mpaka kesho savo, Taita Taveta," Nyoro alisema.

Ziara ya Ruto katika kaunti hiyo ilikuwa ikipangwa takriban wiki mbili baada ya machafuko kutokea eneo la Kenol alipokuwa amehudhuria hafla ya kanisa.

Katika machafuko na vurugu hiyo vijana wawili walipoteza maisha yao, huku vurugu hivyo vikiibua hisia mseto kati ya wakenya na viongozi.