logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanakandanda Victor Wanyama amshtaki mwanasosholaiti Shakilla

Leo hii Wanyama ameposti taarifa ya kusikizwa kwa kesi hiyo

image
na Radio Jambo

Burudani15 October 2020 - 14:33

Muhtasari


  • Victor wanyama kushtaki Shakilla kwa madai kuwa alilala naye
  • Kesi itakuwa katika mahakama ya milimani, mnmo tarehe 10 Novemba 2020
wanyama__1575116037_23539

Gwiji wa kandanda Victor Wanyama hakuwa anacheza wala kufanya mzaha aliposema kuwa atamshtaki mwanasosholaiti Shakilla na mwana blogu Xtian Dela baada ya mwanasosholaiti huyo kudai ya kwamba amelala na Wanyama.

Leo hii Wanyama ameposti taarifa ya kusikizwa kwa kesi hiyo ambayo imepangwa kusikizwa katika mahakama ya Milimani tarehe 10 Novemba mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Wanyama alikana madai hayo ya mwasosholaiti huyo.

Taarifa ya notisi inasoma kama vile ifuatavyo;

"Kupitia kwa notisi iliyotolewa mnamo tarehe 6 Oktoba 2020, kusikizwa kwa mashtaka hayo kutafanyika mnamo tarehe 10 Novemba mwaka wa 2020

Katika mahakama kuu ya milimani saa tatu asubuhi na baada ya hapo kesi itapelekwa katika mahakama kuu ya Nairobi

pata taarifa zaidi kama hautajitokeza, au wakili yeyite wako au mtu ambaye amekubaliwa na sheria mashtaka yataendelea amri zitatolewa kutokuwepo kwako."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved