Jamaa aliyemuua mkewe akamatwa na makachero wa DCI

Muhtasari
  • John alumuua mkewe mnamo tarehe 13 Oktoba na kuingia mafichoni
  • Mshukiwa huyo alikamatwa na makachero wa DCI mnamo tarehe 17 Oktoba

Mshukiwa wa mauaji aliyetoroka baada ya kutekeleza kitendo hicho amekamatwa na makachero wa DCI.

John Mwangi Githaiga,34 alitiwa mbaroni katika eneo la Mathangauta na maafisa wa polisi wa DCI wa eneo la kaunti ndogo Njoro.

Kulingana na maafisa wa polisi John amekuwa mafichoni baada ya kumuua Mercy Njeri Mbatia manamo Oktoba 13.

Huku akitumia kifaa chenye makali inasemekana mshukiwa huyo alimkata shingo Mercy,23 ambaye alikuwa ni mkewe hadi kifo.

"Mwangi ambaye alimkata mwendazake kwa kifaa chenye makali akachoma kichwa, mikono miguu hadi eneo la magoti amekuwa mafichoni na atashtakiwa iwezekanavyo." Ripoti ya DCI Ilisoma.

Mapema wiki hii mshukiwa mwingine aliyemchoma mkewe alikamtwa katika eneo la Kericho alipokuwa anajaribu kutoroka.

Kulingana na ripoti ya DCI John alikamatwa na maafisa wa DCI mnamo Oktoba 17.