Naibu rais Ruto asusia kuhudhuria mkutano wa rais ikulu

Muhtasari

DP Ruto aenda Meru huku akikosa kuhudhuria kikao cha rais Ikulu

Viongozi waliohudhuria mkutano huo waliongozwa na spika Ken Lusaka

Naibu rais aliandamana na viongozi kadhaa katika ziara yake ya Meru

 

 

Image: Hisani

Mpasuko ndani ya serikali ya Jubilee unaendelea kudhihirika huku tofauti za wazi kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake zikiibuka.

Jumamosi Oktoba 17, Rais alikuwa akikutana na viongozi wa bunge la Seneti pamoja na lile la kitaifa.

Hata hivyo, naibu wake hakuwa kwenye kikao hicho kilichofanyika Ikulu na Rais aliketi kwenye meza yake pekee.

Kulingana na taarifa ya Ikulu, ajenda ya mkutano huo ilikuwa Rais kukutana na viongozi wapywa kwenye mabunge hayo mawili ili kujadili miradi ya serikali kuhusu maendeleo.

"Rais Uhuru Kenytata leo alasiri katika Ikulu, Nairobi, alifanya mkutano na viongozi wa mabunge yote wakiwemo viongozi wa kamatai mbalimbali.

Mkutano huo uliandaliwa ili Rais akutane na viongozi wapya kujadili ajenda za maendeleo za serikali." Taarifa ya Ikulu ilisoma.

Viongozi hao waliongozwa na Spika Ken Lusaka wa Seneti na mwenzake wa bunge Justin Muturi.

Ruto alikuwa ameandamana na wanasiasa Mithika Linturi Seneta wa Meru, John Paul Mwirigi mbunge Igembe Kusini, Gichunge Kabeabea Tigania Mashariki, Rindikiri Mugambi Buuri, Raheem Dawood (Imenti Kaskazini), Beatrice Nkatha Tharaka Nithi)na Rehema Jaldesa mwakilishi kina mama, Isiolo.