Kakake Aden Duale azikwa, baada ya kufariki mapema leo katika ajali

Muhtasari
  • Kakake Aden Duale amezikwa baada ya kufariki katika ajali ya barabarani mapema leo
  • Duale alimuomboleza kakake akisema kwamba alichangia sana katika malezi yao
  • Kifo cha kakake Duale kinajiri takriban miezi miwili baada ya mama yao kufariki 
DUALE.1
DUALE.1

Bubow Bare Duale kakake mkubwa wa mbunge wa Garissa Township Aden Duale amezikwa leo katika kaunti ya Garissa.

Dubow ambaye alikuwa amestaafu kutoka jeshi alifariki mapema leo katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Mwingi-Garissa wakati gari lake aina ya Toyota Harrier lilipobingiria.

Baada ya kupokea habari za kifo cha kakake Duale alisema alimtaja Dubow kama mtu mwenye hekima na ambaye alichangia pakubwa katika malezi yake.

Duale alimsifu mwendazake huku akisema ya kwamba alikuwa mtu mwenye kupenda jamii bali..." sisi sote tulitoka kwa Alla na tutarudi kwa Allah".

 

Duale pia alikuwa amesema kwamba kakake angezikwa baada ya swala siku ya Jumapili.

"Kwa kweli sisi ni mali ya Allah na kwake tutarudi kufuatia kifo cha ndugu yangu Haji Dubow Bare Duale, alikuwa na miaka 62. Alikuwa ndugu ambaye alishiriki katika malezi yangu, alikuwa mwenyekiti wa jamii yetu, alikuwa mwenye kupenda jamii. Atazikwa hii leo jioni baada ya maombi." Aliandika Duale.

Naibu rais William Ruto aliwaongoza viongozi wengine katika kumuomboleza kakake Duale.

(Mhariri Davis Ojiambo)