Hustler mgani anatumia helikopta,Wakenya wamwambia Seneta Omanga

senatormillicentomanga
senatormillicentomanga

Seneta maalum Millicent Omanga amejipata pabaya baada ya wakenya wengi kumkejeli, hii ni baada ya kuposti picha akiwa kwenye helikopta na kuambia watu wa Embu kuwa ni wakati wa hustler wa Embu kuwapokea.

Omanga alikuwa anaenda kujiunga na naibu rais William Ruto kwa ziara ya naibu rais katika eneo hilo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliweka picha kuandika ."..Mahustlers Embu tunakam na rieng"  huku wengi wakiuliza iweje maana ya hustler imebadilika.

 

"Mahustlers Embu tunakam na rieng." Aliandika Omanga.

Millicent Omanga
Image: Hisani

Baada ya kusoma ujumbe wa Omanga baadhi ya wakenya walijitosa mitandoani kujibu usemi huo wa Omanga. 

William: Which Hustler flies a chopper??? Danganya wengine wewe mama!

Fenner felix: Hustler and you are in chopper.RUTO and my neighbor share same character traits my neighbor allows only leaves branches dropping in my entrance while friuts NO..... (self explanatory). WAKENYA CHANUKA AMA INUKE

stellah KE: Yaani mtu anakuja na ndege wee unatembea na mguu huna ata baiskeli na akuambia ni hustler kaa wewe??.wakenya ata si wajinga ni maumbwa

Hic sunt: How many ‘Hustlers’ can afford that Helicopter ride?

(Mhariri Davis Ojiambo)