Buriani: Aden Duale aomboleza kifo cha kakake

Muhtasari
  • Aden Duale aomboleza kifo cha kakake mkubwa
  • Mwendazake aliaga baada ya kuhusika katika ajali ya barabara

Aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kitifa Aden Duale anaomboleza kifo cha nduguye aliyefariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.

Kakake mkubwa, Dubow Barre Duale, alifariki baada ya kuhusika kwenye ajali alipokuwa akisafiri kwenye barabara ya Garissa-Nairobi.

Haya yanajiri miezi miwili baada ya mbunge huyo kumpoteza mamake mzazi, ni mwaka ambao utakuwa wa majonzi na kilio katika familia ya Duale.

 

Duru zimearifu kuwa Dubow alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Harrier wakati ajali hiyo ilipotokea.

Marehemu alikuwa mwanajeshi mstaafu ambaye alikuwa amegeukia biashara na alikuwa mmoja wa wafanyibishara mashuhuri mjini Garissa.

Baada ya wakenya kuona habari hizo walitumba risala za rambirambi kwa mbunge huyo na familia yake.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

(Mhariri Davis Ojiambo)