Mke wa pili?

Uhuru azingatia kupata ‘mke’ kutoka Kisumu

'Sijui kama mama nyumbani ataniruhusu.'

Muhtasari

 

  •  Rais aliyasema hayo katika msururu wa ukaguzi wa miradi ya amendeleo huko Kisumu 
  • Rais alikuwa akiwahutubia wakaazi wa Kisumu 

 

 Rais Uhuru Kenyatta amewaacha na kicheko wakaazi wa Mji wa kisumu  baada ya kusema kwamba anazingatia kupata mke  mwingine kutoka mji huo .

"Nilikuwa naambia Raila hapa jameni... Sijui kama mama nyumbani ataniruhusu... Akiniruhusu labda naweza kupata mtu ambaye atakuwa ananitengenezea mambo yangu pande hii..."  alisema huku akicheka .

"Ndio tuwe tukitembea ukijua kuna mahali utakuwa unakula ugali ama namna?"

 Wakati wa hotuba yake  siku ya alhamisi akiwa Kisumu rais alisema mwafaka wa Handshake kati yake na Raila  umempa amani

Uhuru  amesema miaka miwili tangu mwafaka huo ,taifa limeshuhudia  ustawi mkubwa na maendeleo  kinyume na iwapo hawangeamua kushirikiana .

 Akimsifu bwana Odinga  kwa kusimama kidete na mchakato mzima wa BBI  Uhuru amesema Raila Amethibitisha kuwa kiongozi halisi taifa  ambaye aliyeweka  azma  yake kando kwa lengo la  kuisadia Kenya .

 Awali rais alimwelekeza waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi kuhakikisha kwamba   barabara ya kilomita 63 ya Kisumu-Mamboleo-chemelil-Muhoroni inakamilishwa katika kipindi cha miezi mine ijayo .

" Nitarejea hapa Aprili  mwaka ujao  na barabara hii inafaa kukamilishwa kufikia wakati huo’