Hongera! Khaligraph Jones achapisha picha za mwanawe wa kiume

khali-e1471415170725
khali-e1471415170725

Rapper mkali Africa nzima, Khaligraph Jones na mkewe Georgina Muteti wamebarikiwa na mtoto wa kiume kwa jina 'Lu'.

Wawili hao wamekuwa wakichapisha picha za kitinda mimba huyo na kulingana na Georgina, alijifungua mwana huyo takriban wiki mbili zilizopita.

Akitangaza habari hizo njema kupitia mtandao wake wa Instagram, Georgina alifichua kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji wakti alipojifungua kifungua mimba wake, wakti huu kila kitu kilienda salama na alijifungua kwa njia ya kawaida.

Kwa upande wake Khaligraph, alichapisha video akiskiza kibao chake kipya, 'Kwenda' huku akiwa amezingirwa na wanawe wawili.

Tazama picha zifuatazo;

Mkewe Khaligraph
Mkewe Khaligraph