Idadi ya waliombakuziwa Covid-19 yafikia 49,721 baada ya visa 931 vipya kuripotiwa

kagwe
kagwe

 

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 931 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona katika masaa 24 iliyopita.

Kupitia ujumbe uliotumwa kwa vyumba vya habari, visa hivyo vipya ni kutokana kwa vipimo 6,691 vilivyofanywa.

Kufikia sasa visa vilivyoripotiwa nchini sasa vimefika 49,721 kutokana na vipimo vya sampuli 659,920.

Kutokana na kesi hizo 896 ni wakenya huku 35 wakiwa wageni. 615 ni wanaume na 316 ni wanawake.

Kutokana na visa hivyo vipya, mgonjwa mchanga zaidi ni mtoto wa miezi mitano huku mgonjwa mkongwe akiwa na umri wa miaka 90.

Hata hivyo Kagwe alitangaza kuwa watu 6 zaidi wameaga dunia huku idadi ya waliofariki ikifikia 902.

Kagwe aliongeza kuwa watu 333 wamepona kutokana na virusi hivyo huku idadi ya waliopona ikifikia 34,209.