Mwanaume auliwa kwa kuhusika na wizi wa pikipiki

crime
crime

Polisi katika kaunti ya Kirinyaga wanachunguza kisa ambapo mtu mmoja aliuawa kwa madai ya kuiba pikipiki.

Mtu huyo aliripotiwa kuvurutwa kutoka kwa kitanda alipokua amelazwa akipokea matibabu   katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kimbimbi na umati wa watu waliompeleka eneo la Kwa Kariba ambako aliuawa. DCIO  wa Kirinyaga Millicent Ochuka amelaani tukio hilo.

Ifuatayo ni mkusanyiko wa habari tofauti nchini:

Takriban mtu mmoja kati ya wawili humu nchini ana  shinikizo la damu ambalo linaweza kuongezeka, hii ni kulingana na uchunguzi  uliofanywa na shirika moja  hapa Kenya.

Kuongezeka kwa shinikizo la damu huanza  na umri wa miaka 30, idadi ya watu ambayo mara nyingi  imepuuzwa na mipango ya kudhibiti shinikizo la damu.

Watafiti wanasema shinikizo la damu ni ishara ya mabadiliko ambayo yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na shida za figo.

Muuzaji wa gari anayeshtakiwa kwa kulaghai wateja wake zaidi ya shilingi milioni 3.8 atasalia kizuizini mpaka mahakama itakapo amuru kuachiliwa kwake. Mshukiwa, Patrick Aswani, ambaye alikua mafichoni alikamatwa Ijumaa. Mshukiwa anakabiliwa na mashtaka manne ya ulaghai, huku pesa hizo zikiripotiwa kutoka Septemba 2017 na Aprili mwaka huu. Kesi hiyo itatajwa mwezi ujao.

Ikiwa umeolewa chini ya sheria ya kitamaduni,  kunauwezekano kwamba mume wako anaweza kuwa na haki ya kuoa wake wengine. Wakili Rose Mbanya anasema mtu yeyote anaweza kuingia katika ndoa ingine bila ya idhini yoyote. Anasema hata hivyo unaweza kubadilisha muungano wa ndoa yako wa kua na mke mmoja ikiwa utasajili chini ya sheria ya Kikristo au ya Kiraia.

Watu watatu walifariki wakati wengine wawili walipata majeraha mabaya kufuatia mapigano mapya kati ya jamii mbili zenye  ukoo za Garre na Murule katika Kaunti ya Mandera jana.

Mapigano hayo yalizuka Alhamisi usiku na inaaminika kuwa shambulio la kulipiza kisasi. Gavana wa Mandera Ali Roba amelaani mashambulio hayo.