Wakili Philip Nzamba Kitonga aaga dunia

wakili philip Namba
wakili philip Namba

Wakili Philip Nzamba Kitonga ameaga baada ya kuugua kwa muda mfupi, kulingana na familia yake.

Nzamba ambaye aliongoza Kamati ya Wataalam  ya kujadili na kupitia  Katiba ya 2010 aliaga jana jioni wakati alipokua akisafiri kutoka Makueni kuelekea Nairobi.

Nzamba alikuwa miongoni mwa wanasheria walioorodheshwa kumridhi wakili mkuu Willy Mutunga.

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza taifa katika kumuomboleza Kitonga aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 64.

Katika risala yake ya faraja kwa jamaa, ndugu, marafiki na wanasheria nchini, Rais alisema mwanasheria huyo mkuu alikuwa shupavu katika masuala ya kikatiba na mzalendo mahiri wa sheria

Kwingineko, wakili Onesmus Masaku, ambaye  aliaga kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kukatwa mikono na afisa wa polisi Nancy Njeri alizikwa jana nyumbani kwake katika Kaunti ya Machakos huku kukiwa na  ombi la kupata  haki.

Rais wa LSK Nelson Havi amewalaumu polisi kwa kile alichodai ni kuongezeka kwa visa vya mauaji na kushambuliwa kwa mawakili nchini, na pia ametaka uchunguzi wa haraka kufanywa.