Nyamaza kabisa! Murkomen aambiwa baada ya kusema rais ameligawanya taifa

Muhtasari
  • Murkomen alimshtumu rais huku akisema ameligawanya taifa
  • Baadhi ya wakenya walimshambulia Murkomen na kumwambia anapaswa kumuacha rais afanye kazi yake
qiPJWXQt_400x400
qiPJWXQt_400x400

Baada ya Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kumshtumu rais Uhuru Kenyatta kwa kuigawanya nchi kupitia mchakato wa siasa za BBI wakenya wengi walimshambulia huku wengi wakimshauri anapaswa kufyata mdomo.

Kupitia twitter seneta huyo alisema Uhuru anafaa kutumia maafikiano katika kuhakikisha kwamba mapendekezo ya BBI yanapitishwa bila kuzua mgawnayiko miongoni mwa wakenya .

" Nataka kumrai rais Uhuru akome kuligawanya taifa . rais anafaa kuwa kiongozi wa wote na kujifunza kuwanganisha wakenya na sio hii dhana ya ‘utafanya nini’ Murkomen aliandika.

 

Baadhi ya wakenya walimwambia anapaswa kunyamaza na kumuacha rais afanye kazi yake.

Silas chepkeres:Nyamaza kabisa

Alex: Same narrative was being thrown around by TangaTanga adherents that BBI was not real and only Raila was being played by being kept busy