Eric Omondi amkashifu vikali Ezekiel Mutua baada ya kumkejeli

Muhtasari
  • Eric Omondi amuonya Eekiel Mutua dhidi ya kutumia jina lake
  • Mutua alimuambia mchekeshaji huyo kuwa anapswa kujiheshimu kwa yale anafanya kwenye mitandao ya kijamii
eric omondi
eric omondi

Kwa muda sasa mchekeshaji Eric Omondi amekuwa kwenye vichw vya habari baada ya kuzindua studio yake.

Mkurugenzi wa Kenyan Film Classification Board Ezekiel Mutua alimshambulia na kumkejeli Mcheshi huyo huku akimwambia anapaswa kujiheshimu.

Baada ya Eric kuona matamshi yake Ezekiel mcheshi huyo naye alimkashifu vikali huku vita vya maneno vikishuhudiwa kati ya wawili hao.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake Eric Omondi alikuwa na haya ya kumwambia mkurugenzi huyo;

"Dktr Ezekiele Mutua  hii ni onyo yako ya mwisho, hii sio njia ya kuhutubia rais wa bara zima  wacha kutumia jina langu kwa foleni za umma ambazo ni za bai nafuu

Sijawahi fahamu huwa unafanyanya nini ili kukimu maisha yako, haujasaidia tasnia ya burudani kwa vyovyote vile, kwa hivyo ulienda Mombasa kwa ajili ya kuhotubia wanahabari kwa ajili ya hili, si ungenipa pesa hizo niongeze kamera katika studio yangu." Eric Aliandika.

Eric alimwambia Ezekiel anapaswa kutembelea studio zake ili kuona ambayo wana andaa kwa ajili ya vijana.

"Tafadhali tembelea studio za Eric Omondi, na uone ambacho tunatayarisha kwa ajili ya kuwasaidia  vijana wetu na vipaji ambavyo vinachipuka

Usiwahi ongelelea jina langu tena,haujui wala kufahamu hadithi yangu wala kuelewa mchakato wangu."

Tasnia ya burudani humu nchini imekuwa ikibadilika kila kuchao