Miguna Miguna atangaza kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Nairobi

Muhtasari
  • Miguna Miguna atangaza kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Nairobi
  • Alitangaza hayo huku akisema kwamba wale wanataka kumuunga mkono wamekaribishwa
Screenshot_from_2019_12_16_04_21_56__1576488144_66205
Screenshot_from_2019_12_16_04_21_56__1576488144_66205

Wakili Miguna Miguna aliwashangaza wengi baada ya kusema kuwa atawania kiti cha ugavana kayika kaunti ya Nairobi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Miguna alisema kwamba katiba inamkubalisha kuwania kiti chochote cha siasa, pia alifichua kwamba amepata ushauri wa kisheria kupitia kwa wakili Waikwa Wanyoike kuhusu jambo hilo.

Alitangaza hayo huku akisema kwamba wale wanataka kumuunga mkono wamekaribishwa kujiunga na timu yake.

 

"Waikwa Wanyoike na  wakili wengi wa katiba, kupewa mtawala na Uhuru Kenyatta kukataa kuniruhusu kuingia Kenya kwa kukiuka maagizo mengi ya korti

Je katiba hainipi haki kugombea ofisi ya umma kutoka uhamishoni, Baada ya kupokea ushauri mzuri wa kisheria kutoka kwa Waikwa Wanyoike tarehe 19,Desember 2020 

Mimi Miguna Miguna mwananchi wa kenya, na mpiga kura msajiliwa wa kaunti ya Nairobi natangaza uwaniaji kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi Wajitolea wanakaribishwa." Aliandika Miguna.

Mnamo mwaka wa 2017 Miuna aliwania kiti cha ugavana huku akishindwa katika kivumbi hicho.

Haya yanajiri siku chache baada ya gavana Mike Sonko kubaduliwa mamlakani.