'Ninancho ni Kimywa' Mejja amjibu Shakilla baada ya kumkashifu

Mejja na Massawe Japanni studioni
Mejja na Massawe Japanni studioni

Msanii wa kutajika, Mejja almaarufu Okwonkwo, ameamua kumjibu mwanashosholaiti, Shakilla baada ya kushambulia usanii wake.

Mejja na Sauti Sol walishirikishwa katika kibao cha 'Nairobi' kibao chake Bensoul na mwanamitindo huyo aliamua kumshambulia Mejja akisema kuwa yeye ndiye aliyeharibu wimbo huo.

Isitoshe alimuomba Bensoul afute mistari ya msanii huyo kwa wimbo huona kuuweka tena kabla mda hauja yoyoma.

Shakilla aliandika;

"Mtu amwambie Mejja si lazima kwake kushirikishwa katika kila wimbo,kibao cha Nairobi kilikuwa kizuri hadi pale alianza kuimba mistari yake

 

Anakaa Amin Dada mwenye gharama ya chinisekunde zake tatu hazikuhitajika, wacha mistari yake ifutwe na kibao hicho kiwekwe tena kwenye youtube kabla mda hauja yoyoma."

Baada ya mda mchache shabiki mmoja alimwandikia Mejja yale Shakilla aliyosema na kama kawaida yake, hakumjibu kwa hasira kwani alisema kuwa yeye atasalia tu kimya na kuendelea kuwa na mda mwema.

"Ninacho ni kimya pekee. Hapa ni good vibes pekee mungu akubariki." Alisema Mejja.

 

Baadaye, alichapisha picha yake akiwa kwenye kanda ya wimbo huo wa Nairobi na kuandika,

Nairobi.............. MLale Poa Wagenge MUNGU AWABARIKI.