Wakenya wanajua nani mnyakuzi wa ardhi,'Ngilu amtetea Kalonzo

Muhtasari
  • Charity Ngilu amtetea Kalonzo dhidi ya madai yake DP Ruto kwamba amenyakua ardi ya NYS
  • Akizungumza siku ya Jumanne alisema kwamba kila mkenya anafahamu mnyakuzi wa ardhi ni nani
  • Pia alisisitiza kwamba Kalonzo alinyakua ardhi hiyo kisheria

Gavana wa kaunti ya kitui Charity Ngilu amemtetea kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kutokana na  madai yake naibu rais William Ruto.

Kulingana na Ngilu DP hana jukwaa la maadili kumfundisha mtu yeyote juu ya maswala ya unyakuzi wa ardhi.

"Madai ya Ruto kwamba Kalonzo alinyakua ardhi ni uongo, kila mkenya anaweza kutambua na kujua nani mnyakuzi mkubwa wa ardhini nani katika nchi yetu kama si duniani." Ngilu alizungumza.

 
 

Wiki jana DP Ruto alidai kwamba kalonzo amenyakua ardhi ya hekari 200 katika eneo la Yatta ni shamba ambayo ilikuwa ni ya National Youth Service.

Ngilu alisisitiza kwamba Kalonzo alichukua ardhi hiyo kupitia kwa sheria.

Kalonzo pia alikana madai hayo na kusema kwamba yuko tayari kuchunguzwa na kuhojiwa kwa ajili ya shamba hilo.