Bakari Magara amekuwa kama mtoto katika mtaa wake huku akichekwa na kila anayefahamu masaibu yake . Bakari alikuwa na maisha mazuri na mke wake Zura katika eneo la mpeketoni wakati wakiendesha mkahawa wao uliokuwa maarufu katika sehemu hiyo .
Bila kujua kwamba yalikuwa yamemngoja mbele , Bakari aliamua kukwepa kwenda Lamu na mke wa pili ,msichana kutoka Shela ambaye walikuwa wamekula njama kutoroka na kuanza upya maisha mbali na sehemu hiyo ambako walijulikana wote .
Mke wake wa kwanza aliaca na mshangao mkubwa sana wakati zilipoanza kuthibitishwa habari kwamba ni kweli mume wake amemuacha ili kuanza maisha na msichana mdogo . Naye hakuvunjika moyo kazi yake pale mkahawnai aliendelea kuifanya na hata wenyeji kwa sababu ya huruma waliendelea kumletea pesa ikawa sasa shughuli zake za kibiashara zimeoga kweli asieweze kuteseka wka sababu ya kuachw ana mume .
Bakari mambo hayakumwendea vizuri kama alivyotaraji kwani kazi aliofiriki ataipata kule Lamu ikawa haimfai na mwenzake yule mke wa pili baada ya kupata uja uzito akawa mnyonge wa afya na magonjwa yakaanza kumuandama . Isitoshe ,pazuka uvumi kwamba hata ile mimba haikuwa ya Bakari kwa sababu yule mke wake wa pili alikuwa mkaribu huko walikohamia huku wakisema watu kuhusu visa vya wanaume wengine kujihusisha naye wakati Bakari hakuwepo .
Watu walishangaa itakuaje mwanamme mwenye umri kama wa Bakari na heshima zake kumuacha mke wake bila sababu kwa sababu hakukosana hata na mkewe na kutoka kwake kulikuwa kutoroka hasa . Mwanzoni ,hata familia yake ilifikiri katekwa nyara au kapotea na wakamtafuta ikiwemo hata kuripoti kwa polisi . Ilikuwa ni mshangao kwa wote waliomjua kufahamu kwamba jamaa hakufukuzwa wala kukosana na mkewe bali alivutiwa na urembo wa mwanamke wa pil aliyemfanya kuchachawika na kuiacha familia yake mpeketoni .
Bakari alipopata kuthibitisha kwamba mke wake wa pili alikuwa kabeba mimba lakini sio yake , alijua ulimwengu wake kweli ulikuwa umekwisha ,alianza kujutia na kapiga moyo konde kuanza tena kumrudia mke wa kwanza akitokwa machozi na kuomba msamaha . Walioua yote wakikusimulia huruma alioonyesha pale mjini ,kwenye hoteli ya mkewe akitaka kusamehewa ,wanasema ilikuwa kama filamu ya kiafrika ,machozi ,vicheko na majuto .