'Ukiendelea kukosoa serikali jiuzulu,'Rais Uhuru awaambia wakosoaji

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta awataka wakosaji wake wajiuzulu badala ya kukosoa serikali
  • Washirika wa Naibu Rais William Ruto wamekuwa wakikosoa baadhi ya maamuzi yaliyotolewa na serikali ya Jubilee
Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa, Februari 12, aliwataka wakosoajiwa serikali kujiuzulu badala ya kukosoa serikali.

Baada ya kuzindua kliniki ya afya huko Uthiru, Kenyatta alisema hakuna njia wakosoaji wake wanavyokosoa utawala wake na wakati huo huo kujipatia sifa kwa mafanikio ya Jubilee.

 "Ikiwa unahisi serikali ni nzuri, kaa nayo. Ukiendelea kukosoa, ondoka na waache wengine waendelee kufanya kazi. ”

 

Lengo letu ni umoja wa watu na sio kugawanyika. Tunataka watu waendelee kama kitu kimoja. Tunataka viongozi watakaoshughulikia masuala yanayoathiri Wakenya na sio siasa za kugawanya, ”Rais alisema.

Washirika wa Naibu Rais William Ruto wamekuwa wakikosoa baadhi ya maamuzi yaliyotolewa na serikali ya Jubilee.

Ruto mwenyewe ameelezea wasiwasi wake juu ya BBI na kuahidi kutoshiriki katika kura ya maoni ikiwa itakuwa na mgawanyiko.

Siku ya Ijumaa, Kenyatta alisema hatashiriki mapigano ya kisiasa yasiyo ya lazima na kuwashutumu wakosoaji wake kwa kusema mara mbili.

“Huwezi kusema kwa kinywa hicho hicho serikali ni mbaya na pia unasema tumefanikisha hiki na kile kama serikali. Tuna serikali ngapi? ” Aliuliza.