Wakenya Sasa wanaweza kuripoti vyeti bhandia kupitia mtandaoni . Katika njia hii mpya mtu yeyote anaweza tumia tovuti kuripoti visa vya vyeti bandia kupitia tovuti [email protected]/cheti-mwitu.
Kwa mujibu wa mkurungezi mkuu wa Shirika hilo Bwana Juma Mukhwana,njia hii itawezesha kumaliza vyeti bhandia vya masomo humu nchini
Watu nchini wamekuwa wakipata vyeti bandia kama vile vyeti vya shule mara kwa mara.
Mkurugenzi Juma alisema kwamba baada ya mtu kuripoti kuwa kyeti chake kimeibiwa na kutumiwa na mtu mwingine watachunguza madai hayo kwa kina.
"Tumezindua mbinu ya kuthibitisha vyeti bandia inayofahamika kama 'Vyeti mwitu, mtu anaweza ripoti kupitia kwenye tovuti na kisha tutachunguza zaidi
Itasaidia pia watu kugundua vyeti bandia," Alisema JUma.