Rais Uhuru Kenyatta amuomboleza mbunge wa Juja Francis Waititu

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amuomboleza mbunge wa Juja Francis Waititu
  • Waititu aliaga dunia Jumatatu Februari 22, alipokuwa anapokea matibabu ya saratani ya ubongo
Rais Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa rambi rambi kwa familia, jamaa na wakaazi wa eneo bunge la Juja kufuatia kifo cha Mbunge wao Francis Munyua Waititu.

Mbunge huyo ambaye ni mwanachama wa Jubilee aliaga dunia kutokana na saratani ya ubongo Jumatatu usiku katika hospitali ya Mp Shah Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

KUpitia kwenye ujumbe wake rais alimsifu mwendazake, huu hapa ujumbe wake rais.

"Kwa masikitiko tumepoteza kiongozi aliyeenzi maendeleo, aliyeaminika na aliyejitolea kutokana na vitendo vyake vya wananchi aliowaongoza

Ni kwa sababu ya uaminifu na upendo ambao watu wa Juja walikuwa nao kwa Waititu ndio walimkabidhi muhula wa pili katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa licha ya ugonjwa wake," Rais alisema.

Kifo cha Wakapee kinajiri takriban siku saba baada ya kifo cha mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka.