Mtangazaji wa zamani wa habari wa NTV Winnie Mukami ameaga dunia,Kulingana na ripoti, Mukami alikuwa ameambukizwa virusi vya Covid-19.
Aliteuliwa kwa Bodi ya kenya pipeline mnamo 2018 kwa kipindi cha miaka mitatu, Mukami aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi Women.
"Nimepata habari tu kwamba tumepoteza mwanahabari mwenzetu, mwanahabri wa zamani wa NTV Winnie Mukami.
Natuma rambi rambi zangu kwa familia yake na marafiki anapopumzika," Mhariri Olver Mathenge aliandika.
Wakati akifanya kazi katika kampuni ya Nation Media Group ambapo nyota yake iliangaza na mara nyingi alikuwa akilinganishwa na wanahabari wa juu kama Katherine Kasavuli, Swaleh Mdoe, Sophie Ikenye, na Louis Otieno kati ya wengine.
Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.