Nimefurahi sana kwa ajili ya mtoto wangu-Baba yake Faith azungumza baada ya matokeo ya KCPE

Muhtasari

Faith MUmo azungumza baada ya matokeo ya KCPE

Waziri wa Elimu George Magoha Alhamisi, Aprili 15, ametangaza matokeo ya mtihani wa shule za msingi (KCPE) huko Mtihani House jijini Nairobi

Waziri wa Elimu George Magoha Alhamisi, Aprili 15, ametangaza matokeo ya mtihani wa shule za msingi (KCPE) huko Mtihani House jijini Nairobi.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Magoha alibaini kuwa utendaji wa jumla katika 2020 uliboreshwa ikilinganishwa na ile ya 2019.

Mumo Faith kutoka shule ya msingi ya Kari Mwailu aliongoza kwa alama 433, huku akiwa mwanafunzi bora katika mtihani wa KCPE wa mwaka wa 2020.

 
 

Paul Mumo baba yake Faith akizungumza na radiojambo alisema kwamba amefurahi kwa ajili ya mwanawe.

Pia alimshukuru Mungu kwa kumwezesha mwanawe na kuwa bora katika mtihani wa KCPE.

Alikuwa na haya ya kusema;

"Nimefurahi kwa ajili ya Faith, pia namshukuru Mungu kwa kumwezesha, faith ni mwanafunzi na mwana mwema na mwerevu, wakati wa corona tulikuwa tunamuhimiza asome kwa ajili ya mtihani

Ata aliyekuwa mwalimu wake mkuu alikuwa ametuambia kwamba Faith ataongoza katika mtihani wa KCPE," Alisema Mumo.

Pia Faith akizungumza alisema kwamba hakutarajia kuwa ataweza kuongoza katika mtihani wake.

"Nimefurahi sana kwa matokeo yangu, sikutarajia kwamba nitaongoza, lakini nawashukuru wazazi wangu kwa kuniunga mkono,"