Rais Suluhu na Kenyatta wakubaliana kutatua vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na Kenya

Muhtasari
  • Mwanzo mpya katika uhusiano wa nchi ya Tanzania na Kenya umeonekana baada ya rais Suluhu kuzuru nchini siku ya Jumanne
  • Suluhu alisema alifurahi mapokezi ambayo Kenya ilimpa akisema inaashiria umuhimu wa ziara hiyo
Image: PSCU

Mwanzo mpya katika uhusiano wa nchi ya Tanzania na Kenya umeonekana baada ya rais Suluhu kuzuru nchini siku ya Jumanne.

Rais Uhuru Kenyatta na mgeni wake, Rais wa Tanzania Samia Suluhu, walisema walikubaliana kuboresha uhusiano katika biashara, miundombinu, usafirishaji, utalii, utamaduni na usalama kati ya nchi hizo mbili.

Akiongea Ikulu jijini Nairobi baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na Suluhu, Uhuru alisema hata waliwaamuru maafisa wakuu wa serikali kutoka nchi hizo mbili kushirikiana kila wakati ili kuimarisha uhusiano.

 

“Tumewaagiza mawaziri wakutane mara kwa mara kusuluhisha maswala ambayo yanasababisha shida kwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Tunataka kurahisisha kila kitu kwa mataifa haya mawili, ”alisema.

Suluhu alisema alifurahi mapokezi ambayo Kenya ilimpa akisema inaashiria umuhimu wa ziara hiyo.

Alisema nchi hizo mbili zinahitaji kuboresha uhusiano kwani zinagawana mpaka mrefu, na Kenya ikiwa mwekezaji mkubwa wa tano nchini Tanzania, ulimwenguni, na nambari moja katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Suluhu alisema kuna uwekezaji mkubwa wa Kenya 513 nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.(Shilingi bilioni170).

Kuna kampuni 30 za Tanzania nchini Kenya zinazoajiri watu wapatao 2,600