Mwanasoshalaiti Amber Ray alazwa hospitalini

Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray, amelazwa katika hospitali ya Agha Khan Nairobi.

Amber Ray anasema kuwa kuna 'kitu' ambacho alitumia kupita kiasi na hilo ndilo lilisababisha kulazwa kwake.

Hata hivyo alihakikishia mashabiki, jamaa na marafiki kuwa anaendelea kupata nafuu na hayuko hali mbaya.

Huku akichapisha picha akiwa hospitalini, Amber Ray aliandika;

Msijali wadau Niko poa, ile kitu mimi utumia ndio kidogo nili overdose but @akuhnairobi wamei dilute 🤣.

Tazama picha ifuatayo huku tukimuombee apate nafuu ya haraka.