Terence Creative afichua kuwa ananyimwa uwezo wa kuwaona wanawe

Terence.Creative.696x332
Terence.Creative.696x332

Mchekeshaji Terence Creative amewashtua mashabiki wake alipofichua kuwa amenyimwa uwezo wa kuwaona wanawe wawili na aliyekuwa mkewe, Eunice Waneta.

Kwa wale wasiojua, Terence na Eunice Waneta walikuwa kwenye ndoa na walijaliwa watoto wawili wa kike wa miaka 13 na 9 mtawalia.

Terence alifichua haya kwenye kitengo cha maswali na majibu na mashabiki wake katika mtandao wa Instagram.

Alisema kuwa hajawaona wanawe kwa mda sasa kwani amezuiwa kuwaona. Isitoshe alisema kuwa wanawe wamebadilishwa shule na hilo limefanya mambo kuwa mazito.

Mwanzo alikataa kujibu maswali kuhusu wanawe huku akisema ni jambo linalomuumiza moyo, kabla ya kujibu hatimaye.

Shabiki mmoja alipomuuliza kama yeye huwatembelea wanawe alisema;

Okay sawa, mimi huwatembelea shuleni kwa sababu mahali walikuwa wanaishi walihama na sijui wanakoishi saa hii, mmoja alichenjiwa shule yenye nilikuwa najua, saa hii sijui anasomea wapi and the other anasomea Nakuru so nikitaka kumuona lazima niende huko, nauma saana hata baada ya kuwa a good dad and a provider bado nanyimwa shared custody.

Aliongeza;

Katika miaka saba wamekuja kwangu mara moja na kutoka hapo ni stress kabisa kuwaona na ndio maana sipendi kuongelea hii story.

 

0488d0b241d5e30bce81083bec5e4db3
0488d0b241d5e30bce81083bec5e4db3

Tazama baadhi ya maswali aliyoulizwa;