VIRUSI VYA KORONA

India yaagiza mitandao ya kijamii kuondoa kauli 'Virusi aina ya India"

India imesema kuwa jumbe hizo zinazochapishwa mitandaoni ni za uongo na hakuna aina ya virusi inayoitwa 'Virusi aina ya India' iliyotajwa Kisayansi na Shirika la afya duniani(WHO)

Muhtasari

•India  imesema kuwa jumbe hizo ni za kupotosha na zisizo za kweli kuhusu virusi vya Korona

•Aina B.1.617.1   ya Virusi vya Korona ilipatikana kwa mara ya kwanza India mwaka uliopita na imehusishwa na kuua watu wengi sana katika bara Asia.

Mwathiriwa wa Covid India
Mwathiriwa wa Covid India
Image: Hisani:BBC

Serikali ya India imeandikia mashirika yote ya mitandao ya kijamii kuyataka kuondoa kauli 'Virusi aina toka India' ('Indian Variant') kwenye mitandao.

Kupitia ujumbe wa kuchapishwa ulioandikiwa wahudumu wa mitandao ya kijamii, serikali hiyo imesema kuwa jumbe hizo ni za kupotosha na zisizo za kweli kuhusu virusi vya Korona kwenye mitandao.

"Tumejua kuwa kuna kauli inayoenezwa mitandaoni inayosema kuwa virusi vya Korona aina toka India inayosambazwa duniani. Hii ni uongo. Hakuna aina hiyo ya virusi iliyotajwa Kisayansi na Shirika la afya duniani(WHO)" Serikali ya India iliandika

Ujumbe wa India
Ujumbe wa India
Image: Hisani

Aina B.1.617.1   ya Virusi vya Korona (ambalo ni jina lake halisi) ilipatikana kwa mara ya kwanza nchini Idia mwaka uliopita na imehusishwa na kuua watu wengi sana katika bara Asia.India imeagiza mitandao ya kijamii kuondoa kauli hiyo kwa dharura kwani si kauli ya kweli.