USHAURI WA SONKO

(+Picha) Sonko awashauri wanawake kuvumilia mabwana zao

Aliyekuwa gavana wa Nairobi ametumia picha zake akiwa na bibiye wakati hawakuwa wamefanikiwa na pesa kushauri wanawake kuwaheshimu, kupenda na kuvumilia mabwana zao bila kuangazia kazi wanayofanya

Sonko na bibiye
Sonko na bibiye
Image: Facebook

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amewashauri wanawake kuvumilia waume wao bila kuangalia kazi wanayoifanya.

Huku akitumia picha zinazomuonyesha wakiwa na bibi yake Primrose Mbuvi wakati hawakuwa wamefanikiwa na mali mingi kutoa ushauri, Sonko amewahimiza wanawake kuheshimu mabwana zao, kuwapenda na kuwafanya kujiskia kuwa bora zaidi.

Hizi hapa picha alizochapisha Sonko.

"Nyenyekea bila kujali kazi anayoifanya, hakuna hali ya kudumu maishani. Mungu hubadilisha mambo. Kuwa mke mwajibikaji, vumilianeni na Mungu atabariki ndoa yenu siku moja" Sonko aliandika kwenye mtandao wa Facebook.