Je Diamond Platnumz anamsaidia mwanawe Naseeb Junior? Tanasha afichua

Muhtasari
  • Tanasha Donna na mama wa mtoto wa staa wa bongo Diamond Platnumz anaweza kuwa ameweka wazi Diamond  bila kukusudia
  • Alitaka tu kujipa sifa kwa kuwa mama anayefanya kazi kwa bidii ambaye angefanya chochote kabisa kwa mtoto wake
Tanasha
Tanasha Donna Tanasha

Tanasha Donna na mama wa mtoto wa staa wa bongo Diamond Platnumz anaweza kuwa ameweka wazi Diamond  bila kukusudia.

Alitaka tu kujipa sifa kwa kuwa mama anayefanya kazi kwa bidii ambaye angefanya chochote kabisa kwa mtoto wake.

Htaa hivyo wanamitandao na mashabiki wake walisema kwamba ujumbe wake wa kuwapongeza wanawake unaweza kuwa unamaanisha kwamba Diamond hamsaidii mwanawe.

Tanasha ni miongoni mwa wasanii wa kenya ambao hawana ugomvi na wasanii wenzao kwani anazingatia tu kazi yake.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Tansha aliandika ujumbe huu.

"Waheshimu akina mama wote ambao wanafanya chochote kwa ajili ya watoto wao," Aliandika Tanasha.

Ujumbe wake Tanasha unajiri siku chache baada ya Diamond kutoa picha za mwanawe kwenye mitandao yake ya kijamii.

Wawili hao waliachana mapema mwaka jana, baada ya kutoa kiao cha 'Gere'.

Ni ujumbe ambao wanamitandao walimkejeli Diamond kwa kutowajibika.