logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Usipoteze muda wako kusherehekea habari bandia-Atwoli kwa wakosoaji

Picha ya alama kwenye lori iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikichochea uvumi kwamba imeharibiwa.

image
na Radio Jambo

Habari28 May 2021 - 10:22

Muhtasari


  • Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyama vya Wafanyikazi, Francis Atwoli amepuuza madai kwamba alama ya barabara iliyopewa jina lake iliondolewa
atwoli

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyama vya Wafanyikazi, Francis Atwoli amepuuza madai kwamba alama ya barabara iliyopewa jina lake iliondolewa.

Katika taarifa Ijumaa, bosi huyo wa Cotu alisema watu wanapaswa kuacha kupoteza muda kusherehekea habari bandia.

"Hakuna kilichoondolewa kukufurahisha, usipoteze muda wako kusherehekea habari bandia! Matakwa ya Mungu ni ya Juu," Atwoli alisema.

Kauli yake inakuja masaa kadhaa baada ya ripoti kwamba wakaazi wa Kileleshwa wameondoa alama iliyowekwa Alhamisi.

Picha ya alama kwenye lori iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikichochea uvumi kwamba imeharibiwa.

Serikali ya Kaunti ya Nairobi ilitaja barabara kwa jina la Atwoli, katika hafla iliyoongozwa na kaimu gavana, Ann Kananu pamoja na maafisa wengine wa kaunti.

"Ninataka kushukuru uongozi wa Kaunti ya Nairobi, chini ya @annkananu_, kwa heshima hii kubwa na utambuzi wa huduma kwa Serikali ya siku hiyo, jamii na Mfanyakazi kwa ujumla," Atwoli alisema.

Barabara ya Kileleshwa, karibu na Shule ya Upili ya Kenya High, hapo zamani iliitwa Barabara ya Dik Dik.

Pia alidai kwamba matatizo mengi wakenya wanapitia ni kwa ajili ya baadhi ya mawakili, huku akifivhua ugomvi wake na wakili Ahmednasir.

"Matatizo mengi ambayo Kenya inakabiliwa nayo ni kwa sababu ya mawakaili kama @ahmednasir ambaye mkunga rushwa na kutoadhibiwa. Shida zangu na Ahmednasir zilianza wakati nilimzuia kupata malipo haramu kwa NBK. Nitatetea wafanyakazi kila wakati. Siwezi kufanya mikataba na walaghai." Atwoli alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved