Rais Uhuru Kenyatta amuomboleza Kalembe Ndile kama kiongozi aliyetetea haki za wakenya

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amuomboleza Kalembe Ndile kama kiongozi aliyetetea haki za wakenya

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambirambi kwa familia, marafiki na jamaa wa mbunge wa zamani wa Kibwezi Richard Kalembe Ndile aliyefariki Jumamosi usiku.

Katika ujumbe wake wa faraja, Rais alimtaja marehemu Kalembe, 57, kama mwanasiasa mjanja, mwenye dhamira na vitendo ambaye kupanda kwake maishani kulitokana na bidii yake.

"Ni  kwa bahati mbaya kwamba kifo kimemchukua mheshimiwa  Kalembe Ndile katika umri wake. Alikuwa mwanasiasa mchangamfu ambaye alipenda na kufanya kazi na kila mtu, na kila wakati alikuwa na masilahi ya nchi moyoni," Rais alisema.

Kiongozi wa Nchi alikumbuka maingiliano yake na mwanasiasa mjanja zaidi ya miaka akisema, marehemu Kalembe alifanya vizuri kama mpigania haki za binadamu haswa haki ya kupata ardhi.

"Pamoja na kifo cha Mheshimiwa Kalembe, nchi yetu imepoteza mtu aliyekuwa na kipaji cha haki za binadamu. Sote tunakumbuka jinsi alivyopigania shauku ya wanyang'anyi nchini," Rais alimtukuza mbunge huyo wa zamani.

Rais aliitakia familia ya mwanasiasa huyo neema ya Mungu neema na faraja wanapoomboleza kifo chake.