Mhubiri mashuhuri TB Joshua aaga dunia

TB Joshua
TB Joshua
Image: Twitter

Mwinjilisti maarufu wa Nigeria TB Joshua ameaga dunia.

TB Joshua ameaga akiwa na umri wa miaka 57, siku sita tu kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kifo chake kilithibitishwa na kanisa lake la Sinagogi la Mataifa Yote ((The Synagogue Church of All Nations) Jumapili asubuhi.  

Kupitia mitandao yao ya kijami, kanisa hilo lilitangaza;

"Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua kwenda naye nyumbani - kama inavyopaswa kuwa kwa mapenzi ya mungu. Nyakati zake za mwisho hapa duniani zilitumika katika kumtumikia Mungu. Hiki ndicho alichozaliwa, kuishi na kufa." Kanisa lake lilitangaza kifo chake.

Alizaliwa mnamo Juni 12, 1963, huko Arigidi.

Mipango ilikuwa ikiendelea ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Habari za kifo chake zilienea katika mitandao ya kijamii mapema asubuhi ya Jumapili huku wafuasi na wananchi wa Nigeria wakimuomboleza nabii huyo.

Kulingana na taarifa kadhaa, nabii huyo aliugua siku chache zilizopita.