Spika Muturi atetea wadhfa wake kama msemaji wa Mlima Kenya

the star
the star

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi ametetea kutawazwa kwake kama msemaji wa eneo la Mlima Kenya na akawataka viongozi wa siasa kukumbatia tofauti zao.

Muturi anasema eneo hilo litapoteza faida yake ya ushindani iwapo wanasiasa watawagawanya wakaazi, uchaguzi mkuu unapokaribia. Kutawazwa kwake kumezua hisia mseto kwenye eneo hilo.

Kwingineko, mkutano wa Mwangi Kinjuri na wajumbe wa chama chake cha Service Party ulitibuliwa jana na polisi wa kupambaa na vurugu huko Maara, kaunti ya Tharaka Nithi katika kile walichosema ni, kuandaa mkutano wa kisiasa, kinyume cha agizo la serikali la kuthibiti maambukizi ya covid-19.

Kiunjuri alilazimika kuondoka mkutanoni, baada ya vitoa machozi kurushwa. Amelaani hatua hiyo ya kuwatawanya, akiishtumu serikali kwa kushinikiza kanuni hizo kiubaguzi na kutumia polisi kuzima maoni tofauti ya kisiasa.

Hayo yakijiri, Jamii inayoishi katika shamba la Embakasi ranch inaishtumu serikali kwa kutoa ekari elfu 9 za ardhi yao, iliyoko kwenye eneo la Naretunoi huko Kitengelea kinyume cha sheria kwa kampuni za kibinafsi.

Wakiongozwa na mwenyekiti Jonathan ole Lila, anasema walikubaliana na serikali kutumia ekari elfu 3 kwa mradi wa ufugaji kondoo na mbuzi, lakini ardhi hiyo ilikuwa iregeshwe mikononi mwao iwapo mradi huo haungefaulu.

Jamii hiyo sasa inataka kueregeshewa ardhi hiyo, huku kukiwa na hofu ya kupotea kwa ardhi hiyo kwa kampuni za kibinafsi.