Visa vya wanaume kujitoa uhai vimezidi - Utafiti

stress (1)
stress (1)

Upatikanaji wa rahisi wa siaha, na shinikizo la matarajio ya jamii kwamba mwanamume anafaa kuwa jasiri au ataonekana kuwa mdhaifu, huenda ikawa baadhi ya sababu zinazowapelekea wanaume wengi kujitoa uhai, kuliko wanawake.

Mwanasaikolojia Silas Kirinya anasema ingawaje wanawake wengi zaidi hujaribu kujitoa uhai, wanaume wengi zaidi hufanikiwa kwani si rahisi kwao kufunguka, kwa kuogopa unyanyapaa.

tukisalia katika maswala ya wanaume, ni wanaume wachache walio na maradhi ya akili hutafuta usaidizi, kutokana na aibu inayohusishwa na hali hii.

Mwanasaikolojia Silas Kirinya anasema wanaume wanapaswa kuelewa kuwa maradhi ya akii yanaweza kumuathiri mtu yeyote, kwa hivyo kutafuta usaidizi sio ishara ya kuwa mdhaifu.

Kwingineko, watu waliojawa na ghadhabu walimpiga hadi kumuua na kumzika mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 28 anayetuhumiwa kumuua mamake Jumatano usiku, huko Kivingoti, Ndia kaunti ya Kirinyaga.

Mwanamume huyo anasemekana kutoroka na kisha kuregea, akiwa na nia ya kumuua nduguye. Wakaazi wanasema sasa wamepata afueni kwani walikuwa wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa.

Hayo yakijiri, mlalamishi mmoja ameiandikia mahakama ya rufaa, akimtaka rais Uhuru Kenyatta kuwajibishwa kibinafsi kuregesha fedha zilizotumika kuipigia debe BBI, kwa hazina ya kitaifa. Kupitia kwa wakili Morara Omoke, mlamishi huyo pia anaitaka mahakama kumshurutisha rais kulivunjilia mbali bunge, kulingana na ushauri wa aliyekuwa jaji mkuu David Maraga, kwa kukosa kutimiza sheria ya kijinsia ya thuluthi mbili.