MAMA AJIFUNGUA WATOTO 10

Afrika Kusini: Mwanamke avunja rekodi ya dunia baada ya kujifungua watoto 10

Kulingana na bwana ya Sithole, Bw. Tebogo Tsotetsi, watoto hao ambao ni wavulana saba na wasichana watatu walizaliwa kwa njia ya upasuaji siku ya Jumatatu baada ya kubebwa tumboni kwa kipindi cha miezi saba na siku saba.

Muhtasari

•Baada ya uthibitisho wa madaktari, mwanamke huyo atakuwa mama wa watoto kumi na wawili kuona kuwa tayari ako na mapacha wa miaka sita.

•Haya yanatokea wiki chache tu baada ya mwanamke kutoka nchi ya Mali, Halima Cisse, kujifungua watoto tisa katika hospitali moja nchini Moroko mwezi wa Mei.

Gosiame Thamara Sithole na Bwana yake Teboho Tsotetsi
Gosiame Thamara Sithole na Bwana yake Teboho Tsotetsi
Image: Hisani

Mwanamke kutoka nchi ya Afrika Kusini anaaminika kuvunja rekodi ya dunia ya mtu aliyejifungua watoto wengi zaidi baada yake kujifungua watoto kumi.

Ripoti mbalimbali kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa Gosiame Thamara Sithole, 37, alijifungua watoto kumi katika hospitali moja jijini Pretoria.

Kulingana na bwana ya Sithole, Bw. Tebogo Tsotetsi, watoto hao ambao ni wavulana saba na wasichana watatu walizaliwa kwa njia ya upasuaji siku ya Jumatatu baada ya kubebwa tumboni kwa kipindi cha miezi saba na siku saba.

Kulingana na ujumbe ambao Bw Tsotetsti alipatia Pretoria News, awali madaktari walikuwa wamebashiri kuwa bibiye angejifungua watoto wanane jambo ambalo alilitilia shaka sana.

Baada ya uthibitisho wa madaktari, mwanamke huyo atakuwa mama wa watoto kumi na wawili kuona kuwa tayari ako na mapacha wa miaka sita.

Haya yanatokea wiki chache tu baada ya mwanamke kutoka nchi ya Mali, Halima Cisse, kujifungua watoto tisa katika hospitali moja nchini Moroko mwezi wa Mei.