logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DCI yamkamata jamaa kwa kulaghai hopsitali ya Nakuru shilingi 948,000

Baada ya kupokea kiasi chote, mtuhumiwa alitoweka baada ya ahadi kadhaa za uwongo

image
na Radio Jambo

Habari23 June 2021 - 14:12

Muhtasari


  • Jamaa alaghai hospitali ya Nakuru Shilingi 948,000
  • Hospitali hiyo ilifanya malipo ya kwanza ya Shilingi 407,000 kutoka akaunti ya Benki ya Equity kwenda akaunti ya kampuni ya Mwendwa

Maafisa wa upelelezi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wamemkamata Samuel Mwendwa Mutua, 50, kwa kulaghai  hospitali ya St Joseph huko Nakuru.

Kulingana na DCI, Mwendwa alilaghai hospitali hiyo shilingi 948,000, akijifanya atasafirisha vifaa kutoka China akitumia kampuni yake, World Freight Logistics Limited baada ya hospitali hiyo kumpa kazi hiyo  mnamo 2020.

"Vifaa vilijumuisha vitanda vya hospitali, vifaa vya kuhifadhia maiti, vitanda vya kufanyia upasuaji  na kiti cha meno," DCI ilisema.

Mtuhumiwa huyo aliendelea kudai kuwa muuzaji huyo aliyeko Uchina alikuwa ameweka vifaa vyote kwenye kontena lenye futi 40 na inashughulikiwa  kwenye Oceanus Intn'l Logistics (Shenzen) Co Ltd.

Hospitali hiyo ilifanya malipo ya kwanza ya Shilingi 407,000 kutoka akaunti ya Benki ya Equity kwenda akaunti ya kampuni ya Mwendwa iliyofanyika katika benki ya eneo hilo, kama malipo ya ada ya usafirishaji mnamo Novemba 6, 2020.

"Bidhaa hizo zilipowasili nchini Desemba 8, 2020, hospitali ilikuwa imeomba idhini ya kutoka kwa Bodi ya Dawa na Sumu, kabla ya kutolewa Sh158,200 kwa akaunti ya benki ya mtuhumiwa kama malipo ya laini ya kusafirishia na amana za kontena."

Sh383,000 ya ziada ilikuwa Aprili 4, 2021, ilipelekwa kwa mtuhumiwa kuhudumia kodi ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya na ada ya wakala wa Usafirishaji wa Mizigo Duniani, ya mwisho ni Sh183,000," DCI ilisema.

Baada ya kupokea kiasi chote, mtuhumiwa alitoweka baada ya ahadi kadhaa za uwongo kwamba kampuni yake italeta bidhaa hizo katika kituo cha hospitali.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved