logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mpiga picha asimulia alivyoibiwa kamera za 300,000 na wanawake 2 waliompatia dawa za usingizi

Matokeo ya vipimo vya daktari yaliashiria kuwa alikuwa amekunywa dawa aina ya Benzodiazepines.

image
na Samuel Maina

Habari03 July 2021 - 10:46

Muhtasari


  • •Timothy Ndugu almaarufu kama Tim Visuals anadai kuwa wateja wawili walimuitia kazi ya kupiga picha katika jumba la Boon lililo kwenye kijia cha TRM siku ya Jumanne.
  • •Ndung'u alisema kuwa wenye chumba ambacho wanawake hao walikuwa  wamekodishwa  walidai kuwa hawakujiandikisha walipokuwa wanaingia na walipotoka.
Timothy Ndungu

Mpiga picha mmoja jijini Nairobi amejawa na huzuni baada ya wanawake wawili kumpa dawa za kusababisha usingizi kisha kumuibia camera za thamani ya Sh300,000.

Timothy Ndugu almaarufu kama Tim Visuals anadai kuwa wateja wawili walimuitia kazi ya kupiga picha katika jumba la Boon lililo kwenye kijia cha TRM siku ya Jumanne.

Ndungu ambaye anafanyia kazi stesheni moja ya runinga nchini alieleza  kuwa alipofika mahali alipokuwa ameagizwa kupatana na wateja wake walimpatia kahawa ambayo ilikuwa imetiwa dawa za usingizi.

Bila taarifa alikunywa kahawa ile kisha akaanza kuhisi usingizi na akazirai. Hapo ndipo wanawake hao walitoweka na vifaa zake za kupiga picha ambazo anadai kuwa alikuwa amekodishwa.

"Walichukua vifaa zote ambazo nilikuwa nimekodishwa na mpiga picha mwingine anayeitwa Faux Arts na ni za thamani ya 300k" Ndung'u alisimulia.

Ndung'u alisema kuwa wenye chumba ambacho wanawake hao walikuwa  wamekodishwa  walidai kuwa hawakujiandikisha walipokuwa wanaingia na walipotoka.

Alisema kuwa picha za CCTV zilionyesha wawili hao wakiingia na kutoka baada ya kuwa pale ndani kwa kipindi cha masaa mawili.

"Niliamka mida ya saa moja jioni na kila kitu kilikuwa kimechukuliwa"  Alisema.

Kufuatia hayo alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Kasarani na kesi yake ikaandikishwa kama kesi nambari 93/29/6/21.

Matokeo ya vipimo vya daktari yaliashiria kuwa alikuwa amekunywa dawa aina ya Benzodiazepines.

Ametoa wito kwa Wakenya kupiga ripoti wakiona camera za mtumba zikiuzwa kwa bei ya kutupa kwani zaweza kuwa zile alizopoteza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved