Buriani, Rais Kenyatta na Ruto wamuomboleza mwakilishi wadi ya Eldas, Ibrahim Abass

Abass aliaga dunia siku ya Jumapili akiwa Wajir baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Muhtasari

•Rais Kenyatta alimtaja mwakilishi wadi huyo kama kiongozi mwenye maendeleo na ambaye ana uongozi wa mabadiliko.

•Kwa ujumbe wake, naibu rais William Ruto alimtaja kama kiongozi mwenye bidii na maendeleo makubwa. 

MCA Ibrahim Abass
MCA Ibrahim Abass
Image: pscu

Viongozi wakuu nchini, rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamemuomboleza mjumbe wa wadi  ya Eldas  Ibrahim Abass.

Wawili hao wametuma jumbe za rambi rambi kwa jamaa, marafiki na wakazi wa Eldas baada ya kumpoteza Abass ambaye aliaga kufuatia maradhi ya kipindi kifupi.

Rais Kenyatta alimtaja mwakilishi wadi huyo kama kiongozi mwenye maendeleo na ambaye ana uongozi wa mabadiliko.

"Kuaga kwa Bw Abass ni pigo kubwa kwa wakazi wa wadi ya Edas na kaunti ya Wajir. MCA marehemu alikuwa kiongozi mwenye maendeleo ambaye aliweza kutoa suluhu ya matatizo yaliyowakumba watu ambao aliwakilisha kufuatia uongozi wake bora" Rais alisema.

Kwa ujumbe wake, naibu rais William Ruto alimtaja kama kiongozi mwenye bidii na maendeleo makubwa. 

"Inallilahi wainaillahi raijuun, kwake Allah tulitoka na kwake tutarudi. Rambi rambi zangu kwa familia, marafiki na wakazi wa Eldas kufuatia kifo cha mjumbe Ibrahim Abass.

Abbas  alikuwa mwanasiasa asiye wa kawaida, mwenye bidiii na maendeleo. Tuko nanyi katika nyakati hizi za maombolezi. Pumzika kwa amani" Ruto aliandika.

Abass aliaga dunia siku ya Jumapili akiwa Wajir  baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.