Askari akanusha madai ya kumnajisi shemejiye mwenye umri wa miaka 15 Kayole

Muhtasari
  • Afisa mwandamizi wa polisi anayeshtakiwa kwa kumnajisi shemeji yake wa miaka 15 ameachiliwa kwa dhamana ya Shilingi 200,000
  • Sajenti David Kaperia Jumanne alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Makadara Eva Kanyiri
Image: Corazon Wafula

Afisa mwandamizi wa polisi anayeshtakiwa kwa kumnajisi shemeji yake wa miaka 15 ameachiliwa kwa dhamana ya Shilingi 200,000.

Sajenti David Kaperia Jumanne alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Makadara Eva Kanyiri.

Kaperia alikana mashtaka hayo. Kanyiri alimwachilia kwa dhamana ya Shilingi 200,000 na akaamuru suala hilo lisikilizwe mnamo Septemba 22.

Korti ilisikia kwamba mnamo Juni 25 katika eneo la Matopeni huko Kayole kaunti ya Nairobi, afisa huyo alimnajisi mtoto huyo.

Alikabiliwa pia na shtaka mbadala la kufanya kitendo kisichofaa na mtoto.

Afisa aliyeambatanishwa na kituo cha polisi cha Kayole alikamatwa siku hiyo hiyo.

Amekuwa rumande katika kituo cha polisi baada ya korti wiki iliyopita kuwapa maafisa wa upelelezi siku tano kuwazuilia washtakiwa wakisubiri uchunguzi.

Kulingana na nyaraka zilizokuwa mbele ya korti, msichana huyo alikuwa jikoni katika nyumba yao ya makazi akiosha vyombo mnamo saa nne asubuhi wakati mtuhumiwa aliingia ndani ya nyumba hiyo.

Alimshika na kumvuta kwenye chumba cha kukaa ambapo alimvua nguo zake kwa nguvu na kumnajisi.

Mtoto huyo alimfahamisha dada yake ambaye alimpeleka kituo cha polisi cha Kayole ambapo kesi hiyo iliripotiwa.

Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.