UTAENDA NAYE?

Utaenda naye? Mwanamuziki Reuben Kigame kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha urais 2022

Kigame amesema kuwa maafisa wa polisi wamemkataza kufanya mkutano wa kuzindua nia yake leo, Julai 7.

Muhtasari

•Kupitia tangazo alilopakia kwenye mtandao wa Twitter  siku ya Jumanne, Kigame ambaye alipoteza  uwezo wake wa kuona alitangaza kuwa angezindua hadharani azma yake ya kuwania kiti hicho leo(Julai 7)  kati ya saa nne asubuhi na saa sita adhuhuri.

•Hata hivyo kwa ujumbe mwingine ambao ameandika Jumatano asubuhi, Kigame amesema kuwa maafisa wa polisi wamemkataza kufanya mkutano wa kuzindua nia yake.

Mwanamuziki Rueben Kigame
Mwanamuziki Rueben Kigame
Image: TWITTER// REUBEN KIGAME

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Reuben Kigame ameashiria azma yake ya kuwania kiti cha urais nchini Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kupitia tangazo alilopakia kwenye mtandao wa Twitter  siku ya Jumanne, Kigame ambaye alipoteza  uwezo wake wa kuona alitangaza kuwa angezindua hadharani azma yake ya kuwania kiti hicho leo(Julai 7)  kati ya saa nne asubuhi na saa sita adhuhuri.

Hata hivyo kwa ujumbe mwingine ambao ameandika Jumatano asubuhi, Kigame amesema kuwa maafisa wa polisi wamemkataza kufanya mkutano wa kuzindua nia yake.

"Mkutano wa kuzindua nia yangu kuwania kiti cha urais umesimamishwa. Polisi wametuarifu kuwa hakufai kuwana mkusanyiko wa watu leo.  Kejeli gani hii kwa uhuru wa kisiasa ambao tulipata miaka 31 iliyopita! Kaeni mkingoja taarifa nyingine. Bado itafanyika leo" Kigame aliandika.

Kigame ambaye alizaliwa mwaka wa 1966 katika kaunti ya Vihiga alikuja kutambulika sana kutokana na wimbo wake 'Enda Nasi' ambao unaendelea kuchezezwa nchini na nje ya mipaka ya Kenya.